IQNA

Israel inataka kulazimisha mapatano ya fedheha huko Gaza

8:56 - December 31, 2008
Habari ID: 1725266
Mwanachuoni mwandamizi wa Lebanon Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah, amesema lengo la utawala wa Kizayuni katika jinai zake zinazoendelea huko Gaza ni kutafuta njia za kulazimisha mapatano ya kufedhehesha ambayo yataainisha hatima ya Palestina katika uchaguzi ujao utawala huo ghasibu.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Mustaqbal la Lebanon, Allamah Muhammad Hussein Fadhlullah aliyasema hayo Jumatatu alipokutana na Samir Qintar, Mwenyekiti wa mateka wa Lebanon walioachiliwa huru kutoka kwenye minyororo ya Israel. Ameongeza kuwa sababu ya kumwagwa damu ya Wapalestina katika siku za hivi karibuni ni kuwa, utawala haramu wa Israel unataka kuzishurutisha serikali za Kiarabu na jamii ya kimataifa kuhitimisha kadhia ya Palestina kwa kuafiki mapatano ya amani yenye yatakayowabana Wapalestina. Mwanchuoni huo wa Lebanon amesema, pamoja na hayo utawala haramu wa Israel kwa kuendeleza hujuma za kinyama na kutekeleza mauaji ya mara kwa mara, hauwezi kubadilisha mapambano endelevu ya taifa lililodhulimuwa la Palestina.
Amesema, Wazayuni pamoja na silaha hatari walizopewa na Marekani kuangamiza harakati za Wapalestina za kujikomboa, hawataweza kujiondoa katika mgogoro wa kiusalama na kisiasa.
Mwanachuoni huyo wa Lebanon amesema kuwa lengo la makundi mbalimbali ya Kiislamu katika kushiriki kwenye jihadi ni kuyakomboa mataifa yote ya Kiislamu na kushinikiza vikosi vya utawala ghasibu wa Israel huko Palestina na kwingineko katika nchi za Kiarabu na Kiislamu. 341032
captcha