Mkurugenzi wa kituo hicho Hujjatul Islam wal Muslimin Rahim Ja'fari amesema kuwa, maudhui ya kongamano hilo litakalowashirikisha wataalamu na wasimamizi 50 wa masuala ya Qur'ani, ni kudurusu shughuli za Kituo cha Uratibu, Ustawi na Uenezaji wa Shughuli za Qur'ani na taasisi zake hususan suala la elimu na awamu za mitihani ya kitengo cha elimu.
Hujjatul Islam wal Muslimin Rahim Ja'fari amesema kuwa kongamano hilo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa shabaha ya kuwaelimisha wafanyakazi wa Kituo cha Uratibu, Ustawi na Uenezaji wa Shughuli za Qur'ani nchini Iran kuhusu mabadiliko mbalimbali, ratiba na mikakati ya kituo hicho. 341672