IQNA

Malalamiko ya Waaustria dhidi ya jinai za Israel

12:03 - January 03, 2009
Habari ID: 1726502
Makundi 38 ya Kiislamu na ya kutetea amani ya Austria na jumuiya na taasisi mbalimbali nchini humo zimetoa taarifa zikilaani mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Ukanda wa Gaza na zimetaka kufanyike maandamano ya kupinga jinai hizo.
Taarifa hiyo imesema kuwa, raia wa kawaida wanapigwa mabomu bila ya huruma mbele ya macho ya walimwengu na kwamba wananchi wa Gaza ambao wanasumbuliwa na uhaba wa chakula tangu miezi 18 iliyopita kutokana na mzingiro wa jeshi la Israel, wanalengwa kwa mashambulizi ya kinyama ya utawala huo ghasibu na wanainyooshea jamii ya kimataifa mkono wa kuomba msaada.
Taarifa ya makundi mbalimbali ya Austria imeitaka jamii ya kimataifa hususan nchi za Kiarabu, soko la pamoja na Ulaya na Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wao wote kwa shabaha ya kusimamisha umwagaji damu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Taarifa hiyo imesema: Mauaji ya Wapalestina hayapaswi kufanywa gharama ya ushindi wa uchaguzi ujao huko Israel na kwamba serikali ya Austria inapaswa kutekeleza wadhifa na majukumu yake katika uwanja huo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa makundi mbalimbali ya wananchi wa Austria yamefanya maandamano mbele ya ubalozi wa Israel mjini Vienna na mbele ya kanisa kuu la mji huo wakipinga mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina. 342047

captcha