IQNA

Kituo cha mafunzo ya Qur'ani kwa wanawake wa Kuwait chaanzishwa

10:26 - January 04, 2009
Habari ID: 1726876
Kituo cha kwanza cha mafunzo ya Qur'ani Tukufu na lugha ya Kiarabu kwa wale wasiozungmza Kiarabu waishio Kuwait kimefunguliwa katika msikiti mkuu wa Kuwait.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Qabas, kituo hicho kimeanzishwa kwa hisani ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait na kitakuwa kikiendeshwa na Idara ya Mafunzo ya Kiislamu ya wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait Adel Al Falah amesema kuwa, kituo hicho kitakuwa kikitoa mafunzo ya misingi na ufahamu wa Qur'ani, Uislamu na mafunzo ya lugha ya Kiarabu kwa wasiozungumza lugha hiyo.
Ameongeza kuwa ili kuboresha shughuli za kidini na Qur'ani na kutoa huduma bora kwa waliowachache wasiozungumza Kiarabu nchini Kuwait, wizara yake itashirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Kuuarifisha Uislamu pamoja na balozi kadhaa za kigeni katika shughuli zake.
Adel al Falah amesema kuwa taasisi na vyuo vikuu kadhaa vya kidini vya nchi za Kiarabu vimesema vitatuma wahadhiri na suhula za mafunzo kutumika katika chuo hicho. 342462
captcha