IQNA

Waislamu wahujumu mitandao ya Intaneti ya Israel

11:47 - January 04, 2009
Habari ID: 1726887
Kundi moja la Waislamu limeshambulia mtandao wa intaneti wa utawala huo wa Kizayuni wa Israel katika kulalamikia jinai za utawala huo huko Gaza
Kwa mujibu wa toleo la Jumamosi la gazeti la Al-Dastur la Jordan, kundi moja la hackers Waislamu (Watu wanaoshambulia mtandao wa Internet kwa kutumia virusi), limehujumu mtandao wa gazeti muhimu la Kizayuni. Radio ya Israel imetangaza kuwa: "Mtandao wa lugha ya Kiingereza wa gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot umehujumiwa na Waislamu".
Katika hatua hiyo iliyo dhidi ya Waisraeli, Waislamu wamehujumu ukurasa huo na badala ya habari potofu zilizokuwemo, walifanikiwa kupachika picha za Wapalestina wasio na hatia waliouawa hivi karibuni huko Gaza pamoja na taswira za gereza za kuogofya za Marekani huko Iraq. Mtandao huo sasa umerudi katika hali ya kawaida.
Mbali na mtandao huo, mitando mingine ya Kizayuni iliyohujumiwa na Waislamu ni mtandao wa benki ya Kizayuni ya Discount Bank na ule wa gazeti la Kizayuni la Maariv.
Radio ya Israel aidha imetangaza kuwa kundi la wahandisi wa radio wa harakati ya Hamas hivi karibuni walihujumu mawasiliano ya radio ya jeshi la Israel na kufanikiwa kuvuruga mawasiliano kwa siku mbili. 343070
captcha