Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Ban Ki-moon imesisitiza kwamba katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, ana wasiwasi mkubwa na kwamba amesikitishwa na mashambulizi ya nchi kavu ya utawala huo huko Gaza. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala ghasibu wa Israel kudhamini usalama wa raia na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wakazi wa Ghaza.
Katika hujuma ya kijeshi dhidi ya Gaza ambayo imeingia siku ya 10, utawala wa Kizayuni sasa unatumia vikosi vya nchi kavu baada ya kutekeleza mashambulizi haribifu ya anga yaliyopelekea zaidi ya Wapalestina 500 kuuawa shahidi wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Watu wengine karibu 3000 wamejuruhiwa, 600 wakiwa mahututi.
Vilevile imeripotiwa kuwa utawala wa Kizayuni unatumia mabomu mazito mazito pamoja na silaha zilizopigwa marufuku vitani kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Madaktari kutoka Norway wamesema, wamgundua kiwango kikubwa cha madini ya uraniumu hafifu katika mabomu yalioangushwa na Wazayuni huko Gaza. Mabomu yanayotengenezwa kwa uraniumu huwasababishia wahanga magonjwa yasiyotibika kama vile saratani.
Mbali na kuwaua kiholela raia, wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameharibu kabisa zaidi ya miskiti 10, mahospitali, vyuo vikuu, nyumba za raia, shule na idara za serikali. Utawala wa Kizayuni wa Israel umekaidi matakwa ya jamii ya kimataifa yanayoutaka kukomoesha mauaji ya halaiki huko Gaza. 343550