Katika maombolezo hayo, Abdul Basir al-Khalif, msimamizi wa msikiti huo amesema kuwa Mashia na wafuasi wa mafundisho ya Ahlul Bait (as) katika mji huo walikusanyika kwa wingi na kunufaika na mafundisho pamoja na ujumbe wa Imam Hussein (as) kuhusiana na mapambano yake aliyofanya huko Karbala dhidi ya madhalimu waliokwenda kinyume na mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw).
Mahatibu waliotoa hotuba katika maombolezo hayo walizungumzia kwa urefu masaibu yaliyompata Imam Hussein na wafausi wake wachache katika kubainisha mafundisho sahihi ya Uislamu katika kukabiliana na maadui waliotekeleza njama za makusudi kwa ajili ya kutaka kuupotosha Uislamu kwa masllahi yao binafsi. Al-Khalif amesema kuwa maombolezo hayo yataendelea katika msikiti huo hadi tarehe kumi Muharram.
Ni muhimu kuashiriwa hapa kuwa siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharram huchukuliwa na Mashia na wafuasi wa Watu wa Nyumba ya Mtume yaani Ahlul Bait kuwa siku za maombolezo kutokana na kuuawa Imam Hussein (as), mjukuu wa Mtume Muhammad (saw). 343525