IQNA

Kujilinda dhidi ya Uzayuni ni ushindi

15:30 - January 06, 2009
Habari ID: 1728120
Huku akisisitiza kwamba bila ya kujali matokeo ya mashambulio ya kinyama yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, wananchi wa ukanda huo ndio watakaokuwa washindi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba nafsi ya kutetea na kulinda utukufu, izza ya kibinadamu na mapambano dhidi ya dhulma na uchokozi wa maadui wa Kizayuni ni ushindi wa moja kwa moja.
Rais Mahmoud Ahmadinejad amebainisha kwamba, kuwepo kwa mifumo ya kidhalimu ulimwenguni ndicho chanzo cha matatizo yote ulimwenguni na kutaka mifumo hiyo ibadilike na kuwa ya kiuadilifu. Akiashiria uvamizi na mashambulio ya kichokozi ambayo yanaendelea hivi sasa huko katika Ukanda wa Gaza na mengine ambayo yamefanyika katika nchi za Iraq, Afghanistan na Lebanon, Rais Ahmadinejad amesema kuwa, mashambulio hayo yote ya kichokozi na kijinai yana chanzo kimoja tu nacho ni cha madola makubwa ya dunia kufuatilia siasa za kujipanua na kupora mali za mataifa mengine duniani.
Huku akisema kuwa madai ya Marekani na waitifaki wake kwamba wanatetea uhuru na thamani za kibinadamu ulimwenguni ni ya kuchekesha, Rais Ahmadinejad amesema kuwa nchi hizo hujichukulia kuwa ni bora zaidi duiani na zilizo na kila haki na kuyanyima mataifa mengine haki zote zikiwemo za kuishi kwa amani, usalama, uhuru na hata haki ya chakula na tiba. Amesema, kama hakungekuwepo na mifumo kama hiyo ya kidhulma bila shaka hakungetokea duniani mfumo wa kidhulma wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unatenda jinai na mauaji ya kutisha dhidi ya watu wasio na ulinzi bila ya kujali lolote. Rais Ahmadinejad amelishukuru taifa la Iran na hasa tabaka la vijana na wanachuo kwa kufanya maandamano makubwa ya kutetea na kuunga mkono Wapalestina na hasa wakazi wa Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mashambulio makubwa ya kinyama kutoka kwa Wazayuni wasio na huruma. 344035
captcha