IQNA

Wairani wanaoishi Croatia wahuisha maombolezo ya Imam Hussein (as)

15:13 - January 06, 2009
Habari ID: 1728121
Wairani wanaoishi nchini Croatia watahuisha maombolezo ya kila mwaka ya Ashura ya Imam Hussein (as). Maombolezo hayo yanafanyika leo katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Zagreb.
Mkuu wa kitengo hicho amesema kuwa maombolezo hayo yataanza leo usiku wa kuamkia siku ya Ashura na kuendelea hadi kesho usiku. Amesema, wafanyakazi wa ubalozi na kitengo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Wairani wanaoishi katika nchi hiyo watashiriki kwa wingi katika maombolezo hayo.
Hotuba na amali maalumu za maombolezo hayo zimepangwa kufanyika katika ukumbi huo katika usiku huu mtukufu. 344236
captcha