IQNA

Mashindano ya 23 ya Qur'ani ya Nigeria kufanyika leo

11:41 - January 08, 2009
Habari ID: 1728234
Mashindano ya 23 ya Qur'ani Tukufu ya Nigeria yanaanza leo Alkhamisi katika jimbo la Bauchi.
Habari zinasema kuwa majimbo 29 ya Nigeria yamejiandikisha kushiriki kwenye mashindano hayo ambayo yanasimamiwa na viongozi wa jimbo la Edo na Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Uthman Dan Fodio.
Alhaj Uthman Abu Dharr ambaye ni miongoni mwa wasimamizi wa mashindano hayo, amesema kuwa kila moja kati ya majimbo hayo 29 limearifisha washindani 10 katika mashindano hayo. Abu Dharr amesisitiza kwamba, hatua za dharura za kufanikisha mashindano hayo ya Qur'ani zimechukuliwa.
Mashindano hayo yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Viwanda cha jimbo la Bauchi yataendelea kwa kipindi cha siku sita. 344622


captcha