IQNA

Mkutano wa vijana wa Kiislamu nchini Qatar

15:27 - January 10, 2009
Habari ID: 1729007
Mkutano wa kimataifa wa ‘Viongozi wa Kesho’ ambao unawajumuisha vijana kutoka nchi tofauti za Kiislamu utaanza huko mjini Doha, Qatar siku ya Ijumaa ijayo tarehe 16.
Gazeti la nchi hiyo la Peninsula limesema kuwa, washiriki 300 wa makundi mbalimbali ya Kiislamu kutoka nchi 75 za dunia watashiriki katika mkutano huo na kujadili changamoto na matatizo mbalimbali yanayoukabili umma wa Kiislamu katika zama hizi. Lengo la kuandaliwa mkutano huo ni kuandaliwa uwanja wa kupatikana harakati ya kimataifa ya Kiislamu kwa ajili ya kueneza amani, uadilifu na maelewano duniani.
Njia za kutatua matatizo ya Waislamu katika uliwemgu wa leo, uchunguzi wa misimamo ya kupindukia mipaka, kuimarishwa ushirikiano wa Waislamu na nchi za Magharibi na kujaribu kuwasilishwa sura halisi ya amani inayohubiriwa na Uislamu na Waislamu ni mambo yatakayojadiliwa katika mkutano huo. 345604
captcha