Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Emarati WAM, washiriki katika kikao hicho kilichofanyika mjini Vienna walijadili azimio nambari 1860 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo limeitaka Israel kusitisha hujuma yake Ukanda wa Ghaza.
Baada ya kikao chao, mabalozi hao walitoa taarifa na kuelezea masikitiko yao kuwa pamoja na kupasihwa azimio la Baraza la Uslama, utawala wa Kizayuni wa Israel ungali unaendeleza hujuma yake dhidi ya nyumba za raia na misikiti ya Gaza mbali na kuwaua watoto, wanawake na raia wengine wasio na hatia katika eneo hilo.
Mabalozi hao wa nchi za Kiislamu wamesisitiza umuhimu wa kukomeshwa mara moja jinai za Israel. Aidha wameitaka Austria, kama mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama, kuushurutisha utawala wa Kizayuni kukomesha unyama wake huko Gaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria Michael Spindelegger aliyehudhuria kikao hicho mjini Vienna amesema kunafanyika majadiliano ya kimataifa kumaliza jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza. 345804