Waandamanaji hao wametaka kusimamishwa mara moja kwa mashambulio na jinai zinazotekelezwa na Wazayuni dhidi ya raia wasio na hatika katika Ukanda wa Gaza na kutangaza mfungamano wao na wananchi hao.
Atif Khori, Mwalimu Mkuu katika mojawapo ya shule za serikali za mjini Washington amesema kuwa, Wamarekani wanasikitishwa mno kuona jinsi haki za binadamu na jinai za utawala haramu wa Israel zinavyotekelezwa katika Ukanda wa Gaza huku jamii ya kimataifa ikiwa imekaa kimya bila ya kuchukua hatua zozote za maana za kukabiliana na mauaji ya umati yanayotekelezwa dhidi ya watu wasio na hatia katika ukanda huo.
Ban Anderson, mmoja wa watetezi wa haki za binadamu nchini Marekani amesisitiza kwamba utawala wa Israel unatekeleza jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza kwa sababu kuwaua watoto katika vita visivyo vya uwiyano ni kitendo cha jinai za kivita. Amesema, jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu zinapasa kutekeleza majukumu yao na kukata mara moja uungaji mkono wao wa kimaada, kimaanawi na kijeshi kwa utawala huo haramu. Vilevile waandamanaji wametia saini hati yenye kurasa 40 inayolaani na kukemea vikali vitendo vya jinai vinavyotekelezwa na utawala huo dhidi ya raia wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza. 345756