Mufti Malik al Shia'r amesisitiza juu ya udharura wa umoja na mshikamano wa Waislamu na Waarabu katika kukabiliana na Israel ambaye ni adui asiyetambua amani na asiyekuwa na huruma na akasema: Sisi ni umma wa jihadi na tutaendelea kuwa wapigaji jihadi.
Amesema kuwa amani ya uongo ina madhara kwa Waislamu na matokeo yake ni kuuawa shahidi na kujeruhiwa wapiganaji wa jihadi na kwamba wahanga wake wakuu ni watoto wadogo.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo harakati mbalimbali za kuonyesha mfungamano na wananchi wa Ukanda wa Gaza huko Lebanon hususan katika kambi za wakimbizi wa Kipalestina.
Wakati huo huo wanafunzi wa vyuo vikuu vya Lebanon wamefanya maandamano na kuchangisha fedha kwa ajili ya raia wanaozingirwa wa Palestina ikiwa ni harakati ya kuonyesha mfungamano wao na watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza. 345836