An-Ni’ma amesema kuwa shughuli hiyo itaigharimu jumuiya hiyo dola milioni mbili. Amesema, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na ukweli kwamba misikiti hiyo inatumika kama vituo muhimu vya kuimarisha muamko wa umma wa Kiislamu.
Amesema, ili kufikia lengo hilo la kukarabati misikiti iliyoharibiwa katika hujuma ya Wazayuni, jumuiya hiyo italazimika kuomba msaada wa watu wema na wakarimu nchini Qatar. Ameendelea kusema kuwa shughuli ya kuikarabati misikiti hiyo ya Gaza itaanza mara tu baada ya kumalizika mashambulio ya utawala haramu wa Israel na kurejea utulivu katika Ukanda huo. 346896