Mwandishi mashuhuri wa Kiyahudi anayeishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina Amos Oz ambaye ni mpinzani wa mashambulizi ya Israel huko Gaza amesema kuwa mapambano ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas na raia wa Gaza yameizuia Israel kufikia malengo yake na kuendelea vita hivyo kutakuwa na madhara kwa utawala huo.
Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa Islamonline, Amos Oz amesema katika makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti la Yediot Aharonot la Israel kuwa "Kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya Gaza kutawatumbukiza askari wa Israel katika kinamasi kibaya zaidi kuliko kile cha Lebanon. Ameogneza kuwa: "Kuendelea hujuma ya kijeshi huko Gaza kutaitumbukiza Israel katika mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Wakuu wa Israel walitazamia kuwa kwa kushambulia Ukanda wa Gaza na kuzorotesha hali ya kibinaadamu katika ukanda huo, wakaazi wa eno hilo wangechukizwa na serika za harakati ya Hamas, lakini sasa baada ya kupita wiki mbili tangu kuanza hujuma ya Israel, umashuhuri wa Hamas umeongezeka na watu wa Wapalestian wanatumia uwezo wao wote wa kujihami"
Wakati huo huo waandishi na malenga 67 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel wametoa taarifa wakitaka vikosi vya Israel viondoke mara moja huko Gaza na kusitisha mauaji ya kimbari katika ardhi hiyo ya Palestina. 347127