IQNA

Al-Kaaba yaoshwa kwa manukato ya Kashan

11:48 - January 14, 2009
Habari ID: 1730803
Nafasi ya ndani ya Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al-Kaaba imeoshwa kwa maji ya Zamzam, manukato kutoka mji wa Kashan nchini Iran, miski na mivuke ya manukato mengineyo.
Gazeti la Saudi Arabia la al-Watan limeandika kwamba, Khalid al-Faisal bin Abdul Aziz, Amiri wa Makka na wanazuoni pamoja na wasomi wengine wa Kiislamu wameshiriki katika sherehe ya kuoshwa nyumba hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka mara mbili, ya kwanza tarehe Mosi Dhil Hijja na ya pili tarehe 15 Muharram.
Sherehe hiyo inatokana na sunna ya Mtume Mtukufu ambaye katika siku ya kutekwa mji mtakatifu wa Makka, alivunja masanamu yote yaliyokuwa katika nyumba hiyo na hatimaye, akisaidiana na masahaba wake, waliosha na kisha kuipaka manukato nyumba hiyo ili kuiweka mbali na uchafu.
Nyumba ya al Kaaba huoshwa kila mwaka kwa maji ya Zamzam, manukukato kutosha mji wa Kashan nchini Iran na vilevile mivuke mbalimbali yenye manukato ya kuvutia. Kuta zake za ndani pia huoshwa na kupanguswa kwa kutumia vitambaa vyenye manukato na marashi. 347419
captcha