IQNA

Mashindano ya 16 ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu Saudia

15:55 - January 17, 2009
Habari ID: 1732048
Mashindano ya 16 ya kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad (saw) ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Saudi Arabia yanafanyika katika Chuo Kikuu cha Imam Muhammad bin Saud katika mji wa Riyadh.
Msimamizi wa mashindano hayo Abdulmuhsin bin Muhammad bin Muammar amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika katika fremu ya sherehe za kitaifa za turathi na utamaduni wa Kiislamu nchini Saudia. Amesema kuwa mashindano hayo yana sehemu mbili za kuhifadhi Qur'ani na hadithi za Mtume (saw) na kwamba lengo lake ni kueneza utamaduni wa kuhifadhi, kusoma Qur'ani na kuzithamini suna na hadithi za Mtume kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu.
Abdulmuhsin bin Muhammad amesema: Sherehe za kuwatunuku zawadi washindi wa mashindano hayo zitahudhuriwa na Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu wa Saudi Arabia Mut'ab bin Abdullah bin Abdulaziz na viongozi wengine wa masuala ya kiutamaduni wa nchi hiyo. 349314
captcha