Vyombo vya habari vya Aljeria vimemnukuu Waziri wa Waqfu wa nchi hiyo Bu Abdullah Ghulamullah Ashraf akisema kuwa msikiti huo utakuwa na uwezo wa kupokea watu 950 kwa wakati mmoja.
Waziri wa Waqfu wa Aljeria amempongeza Meya na wakazi wa mji wa Safinja kwa kuchagua jina la Gaza kwa ajili ya msikiti huo na kusema kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutangaza mshikamano wao na watu wa Gaza ambao wanauawa kwa umati katika nchi yao wenyewe.
Vilevile Ghulamullah Ashraf ameyataka makundi ya Kipalestina kuungana kwa ajili ya kupambana na adui wao halisi yaani utawala wa Kizayuni wa Israel. 351682