IQNA

Mashindano ya intaneti ya 'utukufu wa Gaza' nchini Kuwait

8:35 - January 24, 2009
Habari ID: 1734710
Mashindano ya intaneti yaliyoandaliwa chini ya anwani, 'utukufu wa Gaza' maalumu kwa watoto wa Kuwait yanaendela nchini humo kwa ushirikiano wa Idara ya Utafiti wa Kiislamu ya Wizara ya Wakfu.
Maonyesho hayo yana lengo la kuonyesha uungaji mkono kwa watoto wa Gaza ambao wameuawa kinyama katika mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza.
Mkuu wa kitengo cha utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu nchini Kuwait amedokeza kwamba, mashindano hayo yanafanyika kwa madhumuni ya kuwafahamisha watoto wa nchi hiyo jinai walizofanyiwa wenzao wa Ukanda wa Gaza na utawala ghasibu wa Israel na pia kwa madhumuni ya kutoa msaada wa kimaada kwa watoto hao madhlumu.
Watoto wa Kuwait walio na umri wa chini ya miaka 15 vilevile wanaweza kushiriki katika kujibu maswali 15 yaliyoulizwa katika mashindano hayo na hatimaye watakaojibu sahihi maswali 12 kati ya hayo watapata fursa ya kushiriki katika kura ya mashindano hayo. 352267
captcha