IQNA

Maonyesho ya "Morocco katika Quds" yafanyika Rabat

11:34 - January 25, 2009
Habari ID: 1735265
Maonyesho ya picha yenye anuani ya "Morocco katika Quds" yamefanyika katika kituo cha utamaduni cha Rabat mji mkuu wa Morocco kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Quds la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Lematin, maonyesho hayo yanayofanyika kwa usimamizi wa Mfalme Mohammad wa Sita wa Morocco na mwenyekiti wa kamati ya Quds yanafanyika kwa lengo la kuonyesha nafasi ya Waislamu wa Morocco katika kulinda ardhi za Kiarabu na Kiislamu hasa Quds Tukufu katika zama za Watawala wa Kialawi.
Maonyesho ya "Morocco katika Quds" yanajumuisha picha na nyaraka za kipekee zinazoonyesha historia ya Waislamu wa Morocco huko Quds na ushawishi wao katika kuleta maelewano na mazungumzo ya kidini na vile vile nafasi ya sasa ya Morocco katika kutetea Wapalestina na Quds Tukufu katika nyanja mbalimbali.
Maonyesho hayo yamefanyika katika fremu ya kutangazwa mji wa Quds Tukufu kuwa mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiarabu mwaka 2009. 353395
captcha