IQNA

Warsha ya mafunzo ya uendeshaji wa vituo vya Qur'ani Imarati

11:35 - January 25, 2009
Habari ID: 1735482
Warsha ya mafunzo ya uendeshaji wa vituo vya kuhifadhisha Qur'ani imefanyika Abu Dhabi katika Umoja wa Falme wa Kiarabu ikihudhuriwa na wakurugenzi na wasimamizi wa vituo vya Qur'ani nchini humo.
Shirika rasmi la habari la Imarati (WAM) limeripoti kuwa warsha hiyo imetayarishwa na Idara Kuu ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu katika msikiti wa Sheikh Zayid mjini Abu Dhabi.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Waqfu ya Imarati Muhammad Ubaid al Mazrui' amesema kuwa, lengo la kufanyika warsha hiyo ni kuwaelimisha wakurugenzi na wasimamizi wa vituo vya Qur'ani njia sahihi za uendeshaji wa vituo vya kuhifadhisha Qur'ani, kustawisha shughuli za vyuo vya Qur'ani na kuzidisha mwamko na maarifa ya utamaduni na mafunzo ya Kiislamu.
Amesema kuwa malengo mengine ni kuzidisha uwezo wa mahafidhi na wanafunzi wa vyuo vya Qur'ani katika kuhifadhi kitabu hicho kitukufu, maarifa ya tajwidi na adabu za kusoma Qur'ani na jinsi ya utumiaji wa teknolojia ya kisasa katika uwanja huo. 353016
captcha