IQNA

Mpango wa kuhitimisha Qur'ani nzima katika vitengo 14 vya Qur'ani nchini Iran

10:57 - January 25, 2009
Habari ID: 1735491
Mpango wa taifa wa kuhitimisha kisomo cha Qur'ani katika vitengo 14 vya vyuo vikuu nchini Iran utatekelezwa tarehe 3 Februari sambamba na kuanza sherehe za Waljari 10 za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Umma wa kitengo cha Sayansi ya Qur'ani amesema kuwa mpango wa kuhitimisha Qur'ani tukufu kwa ajili ya kuomba dua ya kudhihiri haraka Imam wa zama Mahdi (as) utatekelezwa tarehe 3 Februari sambana na sherehe za Walfajiri 10 katika vyuo 14 vya Qur'ani nchini Iran.
Muhammad Ridha Basiri amesema, mpango huo unatekelezwa kwa mnasaba wa kuadhimisha miaka 30 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na taathira ya Qur'ani katika mapinduzi hayo.
Vyuo hivyo pia vitajadili mpango wa elimu ya sayansi ya Qur'ani, jinsi ya kujenga uhusiano wa kudumu kati ya vituo vya mafunzo na uhakiki ndani na nje ya nchi na kuitisha semina, mikutano na vikao vya kubadilishana ripoti na uchunguzi katika masuala ya kiutamaduni na elimu ya Qur'ani.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa moja ya kazi za vituo vya elimu ya Qur'ani nchini Iran ni kuchapisha vitabu, magazeti na majarida yenye uhusiano na utamaduni wa Qur'ani na maarifa ya Kiislamu kwa lugha mbalimbali, kutayarisha CD na filamu za mafunzo ya sayansi ya Qurani na kadhalika. 353074
captcha