Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia Sai'd al Arrabi al Harithi amesema kuwa hati hiyo ya ushiriiano inajumuisha mipango ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza na ratiba ya ustawi na ukarabati wa eneo hilo.
Al Harithi amesema, kwa mujibu wa mada za hati hiyo iliyotiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia Nayif bin Adulaziz na mwakilishi wa UNRWA Karen Abu Zayd, shirika hilo litatekeleza mipango ya ukarabati wa eneo la Gaza kwa gharama ya Riyali milioni 24 za Saudi Arabia zilizotolewa na wananchi wa Saudia.
Al Harithi ameongeza kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kudhamini mahitaji ya dharura ya maisha kama chakula, nishati na huduma za matibabu kwa wananchi wa Ukanda wa Gaza.
Saudia Arabia imetia saini hati hiyo ya kuwasaidia wananchi wa Gaza katika hali ambayo viongozi wa nchi hiyo akiwemo Mfalme Abdullah bin Abdulaziz, walikutana kwa siri na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuunga mkono mashambulizi ya jeshi la utawala huo huko Gaza na kuiangamiza harakati ya Hamas. 354425