Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Zambia Muhammad Asadi Muwahhid ambaye pia ni Imamu wa msikiti wa Imam Ridha (as) katika mji wa Lusaka na kuongeza kuwa, kama si juhudi za Imam Sajjad na Bibi Zainab (as) maadui wa Uislamu wangepotosha falsafa ya Karbala na malengo ya mapambano ya Imam Hussein (as) na kuyadhihirisha kuwa ni mapambano yasiyokuwa na malengo ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu.
Asadi Muwahhidi ameashiria taathira za harakati za kiutamaduni za Imam Sajjad (as) katika jamii ya sasa na akasema: Dua za Imam huyo zilizokusanywa katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya ni moja ya vyanzo tajiri mno vya maarifa ya Kiislamu katika dunia ya sasa. Amesema kuwa Risala ya Haki ya Imam Sajjad ambayo inabainisha ufahamu wa juu mtukufu huyo wa masiala ya dini, imeweka wazi haki za serikali kwa raia, haki za raia kwa serikali, haki za mwanadamu na jirani yake na kadhalika.
Ustadh Asadi Muwahhidi amechunguza pia taathira ya hotuba za Imam Sajjad na Bibi Zainab (as) katika kuamsha na kunawirisha fikra za watu. 355145