IQNA

Kuanza duru ya kwanza ya mashindano ya Qur'ani ya Dubai

11:51 - January 28, 2009
Habari ID: 1737038
Duru ya kwanza ya mashindano ya kumi ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu ya Dubai imeanza katika jumba la michezo ya kuigiza la Wizara ya Elimu ya Imarati.
Mkuu wa kamati ya mashindano hayo Ibrahim Muhammad Bumalha amesema kuwa awamu hii ya mashindano ya Qur'ani ya Dubai itawashirikisha wasomaji 205 wa kike na kiume. Washindi katika awamu hii ya mwanzo wataingia katika awamu ya mwisho ya mashindano ya Qur'ani ya Dubai.
Bumalha amesema kuwa, awamu ya mwisho ya mashindano hayo ya kitaifa itafanyika tarehe 14 hadi 23 Februari.
Mkuu wa kamati inayosimamia mashindano hayo ameongeza kuwa sherehe za kutoa zawadi kwa washindi zitafanyika tarehe 25 Februari. Sherehe hizo zitahudhuriwa na mtawala wa Dubai Muhammad bin Rashid al Maktum katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai. 354957
captcha