IQNA

Mfuko wa Kiislamu kuasisiwa nchini Misri

11:45 - January 29, 2009
Habari ID: 1737367
Benki Kuu ya Misri na taasisi muhimu za uwekezaji nchini humo zimekubali ombi la Benki ya Alexandria ya Misri ya kuasisiwa Mfuko wa Fedha wa Kiislamu.
Kuasisiwa kwa mfuko huo ni katika hatua mpya za benki hiyo ya Alexandria za kuimarisha shughuli zake katika soko la hisa na hawala za serikali.
Wawekezaji wakuu wa mfuko huo mpya bado hawajajulikana.
Katika soko hilo la hisa na hawala za serikali, baadhi ya mahitaji ya taasisi na mashirika ya serikali, mabaraza ya miji na mashirika yasiyo ya kiserikali yanaweza kukidhiwa kupitia mikopo kutoka sekta binafsi. 355572
captcha