Kwa mujibu wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Sudan, wasomi na wanasiasa mbalimbali wa Sudan watashiriki katika mdahalo huo unaofanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mfumo wa siasa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, nafasi ya wananchi na wasomi waandamizi wa kidini katika utungaji sheria na maamuzi nchini Iran.
Mwambata a Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu nchini Sudan Ibrahim Ansari atazungumzia nafasi ya Waliul Faqih na nafasi ya Imam Khomeini MA katika kuimarisha wadhifa wa Waliul Faqih katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Aidha Abdul Rahim Omar mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nailin cha Khartoum atazungumza kuhusu namna sheria zinavyotungwa na maamuzi kuchukuliwa nchini Iran. 356375