Kwa mujibu wa gazeti la Ar Rai, kitabu hicho kimeandikwa na Dr. Zaghlul al-Najjar, msomi maarufu wa Qur'ani wa Misri ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu inayoendeshwa na Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Misri.
Mwandishi wa kitabu hicho anazichambua kwa kina sura zote za Qur'ani na kuarifisha nukta muhimu za kisayansi na kiitikadi za Qur’ani.
Katika utangulizi wenye kurasa 30 wa kitabu hicho Dr. Zaghul al-Najjar anaandika kuwa, Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Aya ya 9 Sura la Hijr isemayo: “Hakika Sisi ndio tulioteremsha ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutaoulinda”, anaahidi kuihifadhi Qur'ani Tukufu. Amesema, sababu ya Mwenyezi Mungu kuahidi kuilinda Qur'ani Tukufu ni hii kuwa, mwanadamu bila muongozo wa Mwenyezi Mungu hawezi kutekeleza mafunzo ya risala yake katika ulimwengu kwa mafanikio.
Mtafiti huyu wa masuala ya Qur'ani kutoka Misri amegawa maandishi yake kwa vipengee kadhaa kama vile kuhusu miujiza, itikadi, fiqhi, lugha, ibada, maadili, habari, saikolojia, mafunzo, idara, uchumi na miujiza ya kihistoria ya Qur'ani.
Dr. Najjar ameelezea matumaini yake kuwa kitabu cha ‘Tafakuri Katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu’ kitawezesha vijana Waislamu kufahamu kwa njia bora zaidi aya za Qur'ani, kuhifadhi na kusoma kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu ili kuweza kutumia mafunzo yake katika nyanja mbalimbali za maisha.
Kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu na kina kurasa 567 na ndio kitabu kipya zaidi kulichochapishwa na Dar al-Misriya al-Lubnaniya. 356954