Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Emarati WAM, Walid al Marzuki Mkuu wa kitengo cha utafiti wa Kiislamu cha Taasisi ya Qur'ani Tukufu na Suna ya Mtume (saw) amesema kuwa: “Kitabu hicho ni mjumuiko wa hadithi za Mtume (saw) na washiriki katika mashindano hayo ya kitaifa wanapaswa kuhifadhi hadithi zilizoko katika kitabu hicho”.
Ameongeza kuwa: “Maelezo kuhusu maana ya maneno, istilahi, maana ya hadithi za Mtume (saw) ni kati ya sehemu muhimu za kitabu hicho.
Lengo la kuchwapishwa kitabu hicho limetajwa kuwa ni kuwafahamisha wapenzi wa Suna za Mtume (saw) kuhusu misingi, maana na utekelezwaji wa Suna katika maisha ya kila siku”.
Amekumbusha kuwa Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya na Suna za Mtume (saw) ya Sharjah imeanza kugawa bure kitabu hicho kuanzia Februari Mosi lengo likiwa ni kuwahimiza vijana na mabarobaro kuhifadhi Hadithi za Mtume (saw) na kufahamu maana ya hadithi hizo.
Vitabu hivyo vitasambazwa kote katika Umoja wa Falme za Kiarabu au Emarati. 357447