Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Ismail Hania imesisitiza juu ya kufanyika juhudi zaidi kieneo na kimataifa kwa ajili ya kulijenga upya eneo la Ukanda wa Gaza lililoharibiwa kwa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Taarifa hiyo imeashiria kwamba taasisi nyingi za kiraia, nyumba za wananchi, miundombinu, misikiti na shule ziliharibiwa wakati wa mashambulizi ya kinyama ya siku 22 ya Israel dhidi Gaza, na imezitaka nchi zote duniani kuitisha kikao cha kimataifa kwa ajili ya kutenga fedha zinazohitajika kukarabati eneo la Gaza.
Ismail Hania amesema kuwa hakuna kizuizi chochote cha kuanza ukarabati wa haraka wa Gaza na kwamba serikali ya Hamas inakaribisha nchi zote zilizotangaza kuwa tayari kushiriki katika ujenzi huo kwa njia ya moja kwa moja au kutoa fedha kwa serikali halali ya Hamas.
Taarifa ya Waziri Mkuu wa Palestina imemaliza kwa kusema: Serikali ya Hamas inakaribisha mazungumzo na makundi mbalimbali ya Palestina na kwamba suala linalopewa kipaumbele kwa sasa ni kusimamishwa mashambulizi ya kinyama ya Israel huko Gaza na kujengwa upya eneo hilo. 357414