Abdul Aziz Othman al-Tuweijri, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, amaesifu msimamo wa kishujaa wa Rajab Tayyib Erdogan, Waziri Mkuu wa Uturuki, katika kuwaunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza katika jukwa la hivi karibuni la masuala ya kiuchumi huko Davos nchini Uswisi.
Shirika la Habari la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC lenye makao makuu yake huko Jeddah Saudi Arabia limemnukuu al-Tuweijri akisema kuwa, Erdogan alichukua hatua ya kuondoka kwa hasira katika jukwa hilo katika kulalamikia hatua na matamshi ya uongo ya Rais Shimon Peres wa utawala haramu wa Israel katika kujaribu kuhalalisha jinai za utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza. Amesema, kitendo cha kutopewa wakati wa kutosha Erdoga kwa ajili ya kujibu jinai za utawala huo huko Gaza, ni ishara ya wazi inayothibitisha upendeleo wa nchi za Magharibi kwa utawala huo na hivyo kufunika jinai zake za kivita dhidi ya watu wasio na ulinzi.
Al Tuweijri Amesisitiza kwamba, ulimwengu unapasa kutambua vyema kwamba utawala huo haramu pamoja na lobi za Kizayuni zimepenya na kijiimarisha katika mashirika na taasisi muhimu za kimataifa za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, likiwemo Jukwaa la Kiuchumi la Davos, kwa lengo la kuzuia ufichuliwaji ukweli wa jinai zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia huko Palestina.
Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO amesema kwamba, matamshi ya Erdogan kuwa utawala wa Kizayuni una ujuzi na uzoefu mkubwa katika kuwaua watoto, ni ishara ya wazi kwamba utawala huo inatekeleza mipango ya makusudi na iliyopangwa awali kwa lengo la kuushambuli Ukanda wa Gaza.
Al-Tuweijiri hatimaye amesema kuwa, uungaji mkono kwa watoto wa Palestina dhidi ya mauaji, njaa, mzingiro na kunyimwa elimu ni miongoni mwa majukumu muhimu ya ISESCO na amezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kusifu msimamo wa kishujaa uliochukuliwa na Waziri Mkuu wa Uturuki dhidi ya Peres katika kikao cha Davos. 357953