Shirika la Habari la Imarati (WAM) limeripoti kuwa Mtawala wa Dubai Sheikh Muhammad bin Rashid Aal Makhtum, Mjumbe wa Baraza la Benki ya Kiislamu ya Dubai Sulaiman al Mazrui na Mkuu wa Baraza la Utendaji la benki hiyo Ibrahim Faiz Shami wamehudhuria sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo katika jiji la Dubai.
Mkuu wa Baraza la Utendaji la Benki ya Kiislamu ya Imarati Ibrahim Faiz amesema kwamba ufunguzi wa Benki ya Kiislamu tawi la Dubai ni hatua muhimu kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha na kibenki kwa raia wa Imarati kwa mujibu wa misingi na sheria za Kiislamu.
Ameongeza kwamba suhula zitakazotolewa na benki hiyo kwa wateja wake zitategemea faida itakayotokana na uwekezaji wa pamoja bila ya riba.
Benki ya Kiislamu ya Dubai ni tawi la Benki Kuu ya Kiislamu ya Imarati yenye makao yake Abu Dhabi, mji mkuu wa Imarati. 358738