IQNA

Kuanza mashindano ya Qur'an kwa wanachuo wa Libya

10:04 - February 04, 2009
Habari ID: 1740016
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani kwa wanachuo wa Libya yameanza huko katika mji wa Sirt kaskazini mwa Libya.
Kwa mujibu wa tovuti ya ljbc.net, mashindano hayo ambayo yataendelea kwa muda wa siku tatu yatawajumuisha wanachuo 40 wa vituo vya kuhifadhi Qur'ani nchi Libya.
Mashindano hayo yanafanyika katika makundi mawili ya wanaume na wanawake ambapo washiriki watatakiwa kuhifadhi ima Qur'ani nzima, juzuu 15, juzuu, saba na juzuu tano za mwisho za Qur'ani.
Muhammad bin Jawad, katibu wa mashindano na idadi kadhaa ya maualamaa, maimamu wa misikiti, mahatibu na wakuu wa vituo vya kuhifadhi Qur'ani vya Libya walishiriki katika sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo.
Kamati inayosimamia mashindano hayo imeandaa zawadi nono kwa washindi wa kwanza hadi tatu wa mashindano hayo. Zawadi hizo zitatolewa kwa washindi Ijumaa tarehe 6 Februari. 358640
captcha