IQNA

Israel yafunga kituo cha Qur'ani kusini mwa Msikiti wa al-Aqsa

10:52 - February 05, 2009
Habari ID: 1740473
Askari vamizi wa utawala haramu wa Israel wameshambulia na kufunga kituo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu kinachoitwa Zaid bin Thabit katika mji mtakatifu wa Quds kusini mwa Msikiti wa al-Aqsa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ma'n, askari hao baada ya kuvamia kituo hicho, waliiba na kupora kila kitu cha thamani kilichokuwa humo na hatimaye kukifunga.
Kwa kufyatua risasi kiholela, askari hao wa Kizayuni walifukuza na kuwazuia Wapalestina wasikikaribie kituo hicho wala kufanya maandamano ya kulalamikia hatua hiyo ya kibaguzi katika kituo hicho cha Qur'ani.
Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel vilevile walimtia nguvuni Sufyan Jadullah, mkuu wa kituo hicho na kukosea heshima nuskha za Qur'ani zilizokuwa katika kituo hicho. 359271
captcha