IQNA

Le Monde: Jamii ya kimataifa imeipuuza Gaza

11:33 - February 05, 2009
Habari ID: 1740481
Gazeti la Ufaransa la Le Monde limechapisha makala iliyobeba anwani ya "Jamii ya Kimataifa Imepuuza Gaza" likichambua utendaji wa jamii ya kimataifa kuhusu hali ya eneo hilo la Palestina.
Sehemu moja ya makala hiyo imesema: Jumuiya za kimataifa hazina azma ya kweli ya kuwafikisha mahakamani viongozi na makamanda wa jeshi la Israel kwa kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Mwandishi wa makala hiyo Saroj Hilmi amesema: Wakati wa mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya Gaza jumuiya na taasisi za kimataifa hazikuchukua hatua za maana za kusimamisha mashambulizi hayo na ziliwaacha peke yao wakazi wa eneo hilo.
Mchambuzi huyo mwenye umri wa miaka 61 wa Kifaransa amesisitiza katika makala ya Le Monde kwamba jeshi la Israel imeharibu hata taasisi na miundombinu ya Gaza iliyokuwa imejengwa kwa misaada ya nchi za Ulaya lakini umoja huo haujachukua hatua yoyote katika uwanja huo.
Ameandika kuwa, wakati wa jinai za Israel huko Gaza, bunge la Marekani lilipasisha azimio likitaja jinai, ukatili na mauaji ya utawala huo dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza kuwa ni hatua ya kujilinda na kwamba hatua hiyo imeonyesha upendeleo usiokuwa wa kiadilifu wa nchi za Magharibi hususan Marekani kwa Israel na mipango yao ya kutaka kuiangimiza harakati ya Hamas.
Makala ya Le Monde imeendele kuwa tangu muda mrefu nyuma Israel ilianzisha mzingiro mkubwa dhidi ya raia wa Gaza na kuzuia dawa, chakula, maji na mahitaji mengine ya dharura kuingizwa katika eneo hilo, lakini Umoja wa Ulaya haukuchukua hatua yoyote ya kupinga hali hiyo.
Mwandishi wa makala hiyo amesema: Misimamo isiyokuwa ya kibinadamu ya Umoja wa Ulaya, Marekani na baadhi ya viongozi wa Kiarabu ya kuunga mkono mauaji ya watu wasiokuwa na hatia wa Gaza, inastaajabisha.
Mwandishi wa makala ya Le Monde amemalizia kwa kuandika kuwa: Wananchi wa Palestina wamelinda moyo wa mapambano na utambulisho wao wa kidini na kitaifa licha ya miaka sitini ya masaibu yanayotokana na dhulma za wavamizi wa Israel na kupuuzwa na jamii ya kimataifa, suala ambalo ni muujiza wa Mwenyezi Mungu. 359373


captcha