Mkurugenzi wa masuala ya kisheria wa CAIR amekaribisha hotuba ya Obama kuhusu suala la kueneza amani na uvumilivu kote duniani akitegemea maneno yenye thamani ya Mtume Muhammad (saw) katika uwanja huo na akasisitiza kwamba: CAIR inatarajia kuona wafuasi wa dini zote wakiheshimiwa duniani hususan Marekani katika siku zijazo na kuondolewa nyufa zilizopo katika medani hiyo.
Alkhamisi iliyopita Rais Barack Obama wa Marekani alihutubia kikao cha wawakilishi wa bunge, shakhsia wa kidini na wawakilishi nchi kadhaa duniani na pamoja na kuzungumzia vipengee vya Taurati na Injili, alinukuu pia hadithi ya Mtume Muhammad (saw) akisema: Katika Uislamu kuna hadithi inayosema: Muislamu wa kweli ni yule anayewatakia wenzake kile anachokipenda yeye.
Obama amesisitiza kwamba, lengo la dini zote ni kuwalingania wanadamu amani, upendo, maisha ya suluhu na kuheshimiana. 360183