IQNA

Taathira za Mapinduzi ya Kiislamu katika mataifa mengine

10:18 - February 08, 2009
Habari ID: 1741591
Mkutano wa "Wimbi la Mashariki” ulioanza jana mjini Tehran umechunguza taathira za Mapinduzi ya Kiislamu katika mataifa mengine.
Mkutano huo unafanyika kwa shabaha ya kuchunguza taathira za Mapinduzi ya Kiislamu katika harakati za ukombozi hususan huko Palestina na Lebanon na jinsi mataifa mengine yalivyofanya mapinduzi hayo kuwa kigezo cha kuigwa.
Kikao cha jana cha mkutano huo kilihudhuriwa na mwakilishi wa wananchi wa Tehran katika bunge la Iran Hussein Fadai na mwakilishi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon nchini Iran Muhammad Hussein.
Sehemu nyingine ya mkutano wa “Wimbi la Mashariki” itahusu maonyesho ya picha za miaka 30 ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, matunda ya mapinduzi na nyimbo zilizotungwa na Hizbullah kuhusu mapinduzi hayo. 360462
captcha