Shirika la Kimataifa la habari la Umoja wa Nchi za Kiislamu IINA limesema kuwa shirika la Saudi Arabia la ar-Rajhi ambalo limeshinda zabuni ya ujenzi wa njia hiyo ya reli litashirikiana na mashirika mengine mawili ya Uchina na Ufaransa kwa ajili ya kujenga na kukamilisha njia hiyo ifikapo mwaka 2013.
Baada ya kukamilika njia hiyo, treni zinazokwenda kwa kasi kubwa ya kilomita 360 kwa saa, zitakuwa zikichukua muda wa nusu saa tu kukamilisha safari hiyo ambayo kwa kawaida huchukua masaa mawili.
Njia hiyo itaboresha zaidi starehe na usalama wa mahujaji na wasafiri wanaosafiri kati ya miji hiyo miwili mitakatifu, wasafiri ambao kwa kawaida hukumbwa na matatizo mengi kutokana na msongamano mkubwa wa magari katika njia hiyo hususan katika msimu wa hija. 361181