Jenerali Yadollah Javani Mkuu wa Idara ya Kisiasa Katika Gadi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amemwambia mwandishi wetu kuwa kimsingi Mapinduzi ya Kiisalmu yanamaanisha harakati ya mabadiliko.
Amesema kuwa mapinduzi yalitokea kutokana na itikadi za kidini za wananchi pamoja na kuwepo viongozi wa kidini. Kwa hivyo wananchi na viongozi wa kidini walitizama matatizo yaliyokuwepo na wakaamua kuwa mwanzo mpya utawezekana tu kwa misingi ya kidini.
Jenerali Yadollah Javani amesema, baada ya kupita miaka 30 sasa ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, irada ya kitaifa ni imara na mfumo wa kisiasa unaotokana na mapinduzi ya kidini umekuwa ukiendelea kwa uongozi wa Faqihi Mtawala na kwa mujibu wa itikadi muhimu zaidi za wananchi, yaani Jamhuri ya Kiislamu. Ameongeza kuwa uhuru wa kisiasa unadhaminiwa nchini Iran.
Afisa huyo wa ngazi za juu jeshiini amesema, pamoja na kuwepo mashinikizo ya madola ya kibeberu, mfumo wa Kiislamu wa Iran unachukua maamuzi yake kwa msingi wa maslahi ya Kiislamu na kitaifa. Amesema, kadhia ya nyuklia ni mfano mzuri wa maamuzi huru yanayochukuliwa na watu wa Iran jambo ambalo limewakasirisha maadui hasa walio katika mrengo wa ubeberu.
Jenerali Yadollah Javani Mkuu wa Idara ya Kisiasa Katika Gadi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa: “Sisi tumechukua mkondo wa uhuru na kujiamini na lango la kuingia hapo ni ezi ya kitaifa. Tunayatetea mataifa yaliyodhulumiwa duniani na tumeweza kufikia ustawi mkubwa chini ya kivuli cha kulinda heshima yetu” 361206