IQNA

15:16 - February 11, 2009
Habari ID: 1743053

Kuhusihwa Arbaini ya Imam Hussein (as)

Marasimu ya kuhuisha Arbaini ya shahada ya Imam Hussein (as) itafanyika tarehe 16 Februari katika miji tofauti ya Australia.

Jumuiya ya Saislamu wa Kishia wa magharibi mwa Austarlia imetoa taarifa ikisema kuwa mwaka huu marasimu ya Arbaini ya shahada ya Imam Hussein (as) yatafanyika katika miji tofauti ya nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa, Imam Hussein si wa Mashia peke yao bali mapambano ya mtukufu huyo, ambayo yalikuwa na ujumbe wa uadilifu, usawa na wema yalikuwa na yangali yana mafundisho muhimu kwa wanadamu wote duniani bila ya kujali rangi, kabila na dini.
Taarifa hiyo inawataka Waislamu wote wakazi wa Australia kushiriki kwa wingi katika marasimu hayo na kuwasilisha kwa walimwengu sura nzuri na halisi ya wafuasi wa Ahlul Beit. Jumuiya hiyo ya Mashia wa magharibi mwa Australia imesema kuwa, lengo la kufanyika marasimu hayo si kutekeleza majukumu ya kidini tu bali shabaha yake muhimu zaidi ni kuwafahamisha watu wasiokuwa Waislamu ujumbe wa kibinadamu na wenye thamani kubwa wa mapambano ya Imam Hussein (as). 362246
captcha