IQNA

Wachina kujenga monoreli ya mahujaji

12:30 - February 14, 2009
Habari ID: 1743901
Kampuni moja ya Kichina imepewa mradi wa kujenga monoreli (treni ya juu kwa juu) katika mji mtakatifu wa Makka.
Kituo cha habari cha Khaima kimeripoti kuwa mradi huo wa kujenga monoreli itakayounganisha mji wa Makka, uwanja wa Arafa na Mina imekabidhiwa kwa kampuni moja kutoka China.
Mradi huo utakaogharimu dola bilioni moja na milioni mia saba, utakamilika katika kipindi cha miaka miwili.
Kampuni hiyo pia itapewa miradi mingine ya ujenzi wa reli katika mji wa Makka ili kusahilisha harakati za mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu. 363232
captcha