Majlisi ya mwaka wa kwanza ya kumkumbuka Shahid Imad Mughnia ambaye alikuwa mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah ya Lebanon imefanyika mjini Tehran ikihudhuriwa na matabaka mbalimbali ya wananchi, viongozi wa serikali, makamanda wa jeshi na mwakilishi wa Hizullah ya Lebanon nchini Iran.
Majlisi hiyo ilihutubiwa na Mwakilishi wa Hizbullah mjini Tehran Ali Zuaitar ambaye amelipongeza taifa la Iran kwa kuadhimisha mwaka wa 30 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa ushindi huo uliyafundisha mataifa yaliyodhulumiwa jinsi ya kupambana na mabeberu.
Ali Zuaitar amesema kuwa shahid Imad Mughnia ambaye alijifunza mengi kutokana na Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kiongozi wake hayati Imam Khomeini alielewa kwamba iwapo mapambano hayataanzishwa dhulma na uonevu utaenea dunia nzima.
Mwakilishi wa Hizbullah nchini Iran ameashiria moyo wa mapambano na kupinga ubeberu wa Imad Mughnia na akasema: Aliweza kulishinda jeshi kubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kuidhalilisha Israel na waitifaki wake.
Amemtaja shahidi Imad Mughnia kuwa ni kigezo bora kilichowatunuku wananchi utukufu na izza na akasema, Mughnia alifanikiwa kuvunja njama za utawala wa Kizayuni wa Israel huku nchi za Kiarabu zikiendelea kuangalia kwa macho utawala huo unaoikaliwa kwa mabavu Palestina kwa kipindi cha miaka 60. 363169