IQNA

Polisi Norway kuvaa Hijabu ya Kiislamu

10:28 - February 15, 2009
Habari ID: 1744180
Serikali ya Norway imeafiki kubadilisha sheria za unifomu za polisi ili vazi la hijab ya Kiislamu liweze kutumika, hatua ambayo imepongezwa na jamii ya Waislamu katika nchi hiyo ya Scandinavia.
Kwa mujibu wa ukursa wa Intaneti wa Islamonline, Ibrahim Bekilani Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Norway amesema: 'Hii ni hatua nzuri kwa ajili ya Jamii ya Waislamu Norway".
Tayari serikali ya nchi hiyo imetangaza kuwa maafisa polisi wanawake wanaweza kuvaa vazi la stara la hijab kwa hiari yao.
Awali Bi. Kulthoum Hasanoui, Muislamu raia wa Norway mwenye asili ya Algeria alikuwa ametuma ombi kwa Wizara ya Sheria akitaka aruhusiwe kuhudumu katika kikosi cha polisi akiwa amevaa hijabu.
Wizara hiyo imejibu maombi hayo kwa kutoa taarifa na kusema: "Baada ya mashauriano na idara ya polisi, imeamuliwa kuwa sheria za sare za polisi zirekebishwe ili kuruhusu uvaliwaji wa hijabu ya kidini pamoja na sare za kawaida".
Bekilani amesema, anatumai sheria hiyo mpya itawatia motisha wanawake Waislamu kuhudumu katika jeshi la polisi la Norway.
Hata hivyo baada ya malalamikio ya baadhi ya vyama vya kisiasa vyenye misimamo ya kibaguzi, polisi ya Norway imesema itachunguza upya amri hiyo. Polisi ya nchi hiyo imedai kuwa vazi la hijabu badala ya kuwashirikisha zaidi wanawake Waislamu katika kikosi hicho itawatenga na kuwaonyesha kuwa jamii ya watu wachache!
Waislamu ni asilimia 15 ya watu takriban milioni 5.3 nchini Norway. Aghalabu ya Waislamu nchini humo wana asili ya Pakistan, Somalia, Iraq na Kaskazini mwa Afrika.
Kwa mujibu wa mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu, vazi la hijab ni wajibu kwa wanawake na wala si nembo ya kidini. Nchi kadhaa za Ulaya ikiwa ni pamoja na Sweden na Uingereza tayari zinawaruhusu maafisa wa polisi wanawake kuvaa hijab. 363790
captcha