IQNA

Chama cha Leba cha Norway chataka maimamu wa misikiti wapewe mafunzo

12:48 - February 15, 2009
Habari ID: 1744183
Chama cha Leba cha Norway kimewasilisha kwa serikali ya nchi hiyo mpango wa kujengwa kituo cha kwanza cha mafunzo kwa wahubiri na maimamu wa misikiti ya nchi hiyo katika Chuo Kikuu cha Oslo, mji mkuu wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Watan, wanachama wa chama hicho wamezitaka serikali za nchi za Kiislamu kushirikiana na serikali ya Norway katika kutoa misaada ya kielimu na kisheria kwa kituo hicho.
Abdul Majid Jarrar, mwanachama wa chama hicho amesema kuwa, katika hali ya hivi sasa, wahubiri na maimamu wengi nchini humo ni wa kigeni ambao hawafahamu lugha wala muundo wa kijamii na kiutamaduni wa nchi hiyo. Amesema, wengi kati ya maimamu hao hutoa mawaidha na darsa zao za kidini na kimuongozo kwa lugha ya Kiarabu, ambayo haifahamiki na raia wengi wa nchi hiyo na hasa tabaka la vijana wazaliwa wa nchi hiyo.
Abdul Majid Jarrar amesema, jambo hilo linasababisha matatizo mengi katika mawasiliano ya kimsingi kati ya pande mbili hizo. 363704
captcha