IQNA

Waingereza wakaribisha huduma za shirika la bima la Kiislamu

17:09 - February 17, 2009
Habari ID: 1745346
Huduma za shirika la bima ya magari la Kiislamu la "Salaam Halal insurance" zimekaribishwa na idadi kubwa ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu nchini Uingereza.
Shirika hilo ambalo linaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria za Kislamu, ni shirika la kwanza la Kiislamu la bima ya magari nchini Uingereza. Licha ya umri wake mfupi, shirika hilo la Salaam Halal ambalo lilianza kazi Agosti mwaka uliopita, limewavutia watu wengi nchini Uingereza ikilinganishwa na mashirika mengine ya bima.
Mbali na huduma za bima kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, huduma za benki kwa mujibu wa sheria za dini hiyo pia zimestawi kwa kiwango kikubwa nchini Uingereza katika miaka ya hivi karibuni kiasi cha kuifanya nchi hiyo kuwa kituo kikuu cha huduma za benki za Kiislamu barani Ulaya.
Kwa sasa benki nne zinazotoa huduma zao zote kwa mujibu wa sheria za Kiislamu zinafanya kazi nchini Uingereza. Vilevile kuna benki nyingine 21 ambazo zinatoa huduma za benki kwa mujibu wa sheria za Kiislamu sambamba na huduma za kawaida za kibenki. 365172

captcha