IQNA

Kikao cha 'Habari za Kidini na Matatizo ya Zama' nchini Tunisia

12:07 - February 18, 2009
Habari ID: 1745466
Kikao cha pamoja cha Wizara ya Masuala ya Kidini ya Tunisia na Wizara ya Wakfu ya Misri kimefanyika huko Tunisia chini ya anwani 'Habari za Kidini na Matatizo ya Zama.' Kikao hicho kimewashirikisha wahadhiri wa vyuo vikuu pamoja na wataalamu wa masuala ya kidini na mengineyo kutoka nchi mbilimbali.
Kwa mijibu wa tovuti ya Allafrika, washiriki wa kikao hicho wamejadili njia mbalimbali za kuimarisha mazungumzo ya kidini na utatuzi wa masuala ya kidini ya zama. Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa kikao hicho cha siku mbili kilichoanza Jumatatu, Waziri wa Masuala ya kidini wa Tunisia amejadili suala la uhakika na mustakbali wa Waislamu.
Kwa upane wake Waziri wa Wakfu wa Misri aliwasilisha makala kuhusiana na maoni na itikadi zisizo na msingi za jamii za Magharibi dhidi ya Uislamu.
Kikao hicho kimefanyika katika sehemu mbili za kuchunguza namna Uislamu unavyoakisiwa katika magazeti ya Kifaransa na Kiingereza na sehemu ya pili ilijadili athari za itikadi katika vipindi vya kidini, vipindi vya kidini katika televisheni za satalaiti zinazotangaza kwa lugha ya Kiarabu, nafasi ya mtandao wa intaneti katika kuchochea tofauti za kimadhehebu na sura ya Uislamu katika intaneti. 365185
captcha