Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa serikali ya Rais Barrack Obama inafanya juhudi za kuboresha sura yake katika Ulimwengu wa Kiislamu, na kwamba serikali hiyo ina azma ya kushirikiana na nchi za Kiislamu kwa ajili ya kupambana na watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka.
Kwa mujibu wa gazeti la Washinfton Post, Hillary Clinton ametoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na wanchuo wa Chuo Kikuu cha Tokyo nchini Japan na kuongeza kuwa, huo ndio mpango muhimu wa Marekani kwa hivi sasa na kwamba kupitia njia ya mazungumzo, serikali ya Washington ina nia ya kuondoa changamoto ambazo zimekuwepo kati ya Marekani na Ulimwengu wa Kiislamu.
Akijibu swali kuhusiana na kuenezwa chuki na woga dhidi ya Uislamu nchini Marekani, Bi Clinton amesema kuwa yeye akiwa Mkrito, ameshuhudia watu wengi katika historia wakitekeleza vitendo vya kinyama kwa jina la Ukristo na hivyo kuharibu jina la dini hiyo. Amesisitiza kwamba, vitendo vibovu vya makundi tofauti havipaswi kuhusishwa na dini wala wafuasi wa dini hizo.
Clinton siku ya Jumatano ameelekea Indonesia, nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani kwa lengo la kuonana na kuzungumza na viongozi wa nchi hiyo. 365864