Mashindano hayo yatafanyika kuanzia tarehe 6 hadi 8 Machi katika mji wa Malmo nchini Sweden.
Habari hiyo imetangazwa na redio ya Sweden ambayo imeongeza kuwa, Baraza la Halmashauri ya mji wa Malmo limechukua uamuzi kuwa duru ya kwanza ya mashindano ya Davis Cup itafanyika bila ya watazamaji kwa sababu polisi haiko tayari kudhamini kwamba itazuia malalamiko ya watazamaji.
Redio ya Sweden imetangaza kuwa mechi kati ya timu za tennis za Israel na Sweden itafanyika katika uwanja wa Baltiska Hallen mjini Malmo ambao una uwezo wa kupokea watu elfu nne.
Wapinzani wa jinai na mauaji yaliyofanywa na Israel huko Gaza wa Sweden walikuwa wametangaza kuwa watasusia shindano la mchezo wa tennis kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Tel Aviv. 366750