IQNA

Argentina, yamfukuza askofu anayepinga holocaust

10:22 - February 22, 2009
Habari ID: 1746951
Serikali ya Argentina imemfukuza nchini humo Richard Williamson, askofu wa Uingereza anayeishi nchini humo kutokana na msimamo wake wa kupinga kile kinachaodaiwa kuwa ni mauaji ya umati dhidi ya Mayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Watan la Saudi Arabia, serikali ya Argentina imedai kuhusiana na suala hilo kwamba upinzani wa Williamson dhidi ya tukio la holocaust unakwenda kinyume na itikadi za jamii ya nchi hiyo, Mayahudi na jamii ya wanadamu. Imempa muda wa siku 10 ili kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Argentina imesema kuwa Williamson amepata umashuhuri mkubwa nchini humo baada ya kupinga holocaust katika mahojiano yake na vyombo vya habari vya Sweden.
Hatua hiyo ya serikali ya Argentina ya kumfukuza askofu Williamson imepongezwa na jamii ndogo ya Mayahudi katika nchi za Latin Amerika. 367128
captcha